A response to another blogger in kiswahili.
PHILIP OCHIENG has a nice take on the killing, "Attacking one's neighbour is misplaced anger.
Ubaya wetu haukuanza na kura tarehe 27, 2007, sisi kila siku tunaona binaadamu wenzetu wakidhulumiwa. Mara ngapi tumesimama na kuangalia kama hayawani mwizi akichomwa na tairi. Ndio wizi ni tabia mbaya, lakini tukifika pahali pakumchoma binaadamu mwenzetu, kwasababu ya shilingi kumi, basi huwa hatuna utu.
Ni jambo muhimu tujiulize, kwanini siku zilizopita hatukuwa na ushujaa na kusema sheria lazima ipewe nafasi, na tuhakikishe wale walio na jukumu hilo la kuhukumu wezi wa aina yeyote, wako na uwezo. Kama wakishindwa kufanya kazi yao, basi hao ndio maadui zetu na kama hatua itachukuliwa, sio huyo masikini mwenzako anafaa kutiwa tairi, bali hao askari, majaji, wana siasa, mawaziri mpaka rais mheshimiwa.
Ukabila upo na sio wakati wa kujadiliana kuhusu ubaguzi, bali tujiulize "utu wetu uko wapi leo." Aibu sio kwa huyu ama yule, Mkikuyu, Mjaluo , Mkalenjin ama Kibaki na Raila, dunia nzima inaona uchi wetu. Aibu ilioje leo. Elimu yetu yote haina faida wala utajiri wakupindukia.
Kanisa linatiwa moto na binaadamu, watoto na kina mama. Bado tunazungumza kama hiyo ni sawa. Muerevu ni yule atakubali kuwa sote tuko na makosa.
Umasikini wakupindukia unatuangalia asubuhi na jioni.
Watoto wa barabarani wanavuta gamu.
Barabara zimejaa mashimo kutoka Busia mpaka Mombasa.
Matajiri na magari ghali vijijini.
Mawaziri wana peleka nguo kufuliwa uingereza.
Ofisi gorofa ya pili, kabila moja.
Kupata kibali kwenda kuja kesho.
Hospitali ya serikali,daktari anauliza “wapi sindano yako.”
Jiji kuu la Nairobi limejaa takataka.
Haina haja kuendelea, hata kipofu atasema, "Harufu mbaya."
Mimi na wewe ndio tulitia moto Kanisani.
Waliokufa kifo kibaya chakusikitisha, sio Wakikuyu.
Tumewauwa ndugu zetu.
Nakuuliza, “sisi ni wageni wa nani leo.”
Raducanu crushed by Swiatek in Melbourne
2 hours ago
No comments:
Post a Comment