Habari Nyote, (Anaglia Kenya Yetu, hawa ni ndugu zetu)
Tafadhali soma.
Hapa Dayton tuko na wakikuyu na wajaluo wengi na makabila mengine kidogo, lakini sote ni wakenya. Najua kuna chuki baina ya wengi. Chuki ambayo haina msingi wakati ndugu zetu wanauana bure.
Natuma barua na picha kila wakati nikijua wengi wanasoma. Sababu kubwa ya kutuma ni kuhakikisha milango ya mawasiliano iko wazi. Jina langu ni Mohamed, ndio mimi ni Muislamu na wengi wenzangu ni Wakristo, lakini ukiuliza mtu yeyote ambaye ananifahamu, atacheka nakujibu, "huyo Mohamed Mkenya." Pia wewe na wengine, majirani wako wanakujua kama Mkenya.
Barua hii singeweza kuandika, isipokuwa tuko pahali pabaya sana wakenya wenzangu. Tusingojee mambo yaharibike kabisa na Kenya kubadilika iwe kama Somalia ama nchi zingine duniani ambazo ziko katika habari kila siku. Najua wengi hawataki Kenya izungumzwe vibaya. Tusimame kama binaadamu walio barikiwa, tufanye kazi ya haki.
Mungu ametuchagua kuwa pahali ambapo tunaweza kufanya makubwa. Tusaidie nci yetu na ndugu zetu. Basi nawaomba musimame tufanye kazi. Leteni maoni.
Kama kazi yako ni kusaidia wengine, simama uisabiwe
Kama wewe ni mwalimu, simama uisabiwe.
Kama wewe ni daktari, simama uisabiwe
Kama wewe ni fundi simama uisabiwe.
Kama wewe ni mwandishi, simama uisabiwe.
Kama wewe ni mwanafunzi, simama uisabiwe.
Kama wewe ni tajiri, simama uisabiwe.
Kama wewe ni masikini, simama uisabiwe.
Kama wewe ni muhubiri, simama uisabiwe.
Kama wewe ni Mkenya, LAZIMA usimame uisabiwe.
MVUKA itasimama iisabiwe. Huu ndio wakati wakutumia MVUKA.
Mola ametubariki na viongozi wazuri walio hakikisha,
"Miami Valley United Kenya Association," iko hai.
Asanteni sana na Mola awabariki,
Mohamed Ahmed
aka: Kamau Onyango
Raducanu crushed by Swiatek in Melbourne
2 hours ago
No comments:
Post a Comment