Kama kweli Kibaki ana utu na kufahamu historia ya dhulma Kenya, basi angeondoka bila ya raia kudhulumiana. Hivi naandika na huku wanaKenya katika mitaa ya Kibera, Kisauni na kwengineko waumizana. Biashara na nyumba nyingi za raia zinawaka moto.
Kwa kweli kulingana na ushaidi kutoka kila pahali, dalili ni wizi usio na mfano wa kura umetokea. Kulingana na habari kutoka Meru, taa zilipotea kwa mda na zilipowaka, kura za Kibaki zilikuwa zimevimba. Basi sio haki kumuita rais mwizi, lakini hakuna shaka wengi watamkumbuka kwa jina baya.
Kwa ufupi Wakenya wamesema, Ukabila hauna pahali Kenya. Wakikuyu ni afadhali waitikie, wasimamae bila ya kuogopa, waseme wao ni wakenya na wanaheshimu sheria.
Kenya sio ya kabila hili ama lile
Kenya sio ya wakikuyu ama wajaluo
Kenya ya leo sio kama nchi zengine za udikteta
Wakikuyu hawana budi, bali kukubali
Kenya ni kubwa na bora kuliko nyumba ya Mumbi
Baba Raila akampa Kenyatta Mkikuyu urais
Mwana Odinga akamsaidia Kibaki, pia mkikuyu
Kumuonda dikteta Moi bila ya kumdhulumu
Basi ni wakati wakikuyu angaa wasimame kwa umoja
Waseme asante sana kwa kuturuhusu kutawala
Waseme kwa sauti kubwa na umoja, si lazima tutawale
Raducanu crushed by Swiatek in Melbourne
2 hours ago
No comments:
Post a Comment